Unordered List

Definition List

Diamond Platinumz Akiuza Domo, Waache BongoFleva Wapige Domo Tu!

Kulingana na taarifa zinazotoka kutoka kwa mtandao wa Millardayo inasemekana kuwa kuna habari za chini chini kwamba single ya ‘number one rmx’ ya Diamond Platnumz ft Davido wa Nigeria ipo kwenye mstari wa kuingiza mihela mirefu kupitia mauzo ya mlio kwenye simu, inasemekana wanigeria wenyewe wanaitaka.

Pamoja na Diamond kutajwa kuwa msanii wa bongofleva anaeingiza pesa nyingi kwa miaka miwili mfululizo kila mwezi kutokana na show zake anazotoza mamilioni ya Kitanzania, mpango mwingine alionao ni kufanya biashara za mavazi kupitia jina lake. Unaambiwa mzigo wa kwanza wa mavazi ya jina lake tayari ulitoka ila aliukataa kutokana na kuwa na kiwango cha chini hivyo ikabidi atoe oda nyingine hukohuko China alikoagiza mzigo wa kwanza.

Pamoja na hizo harakati za kunenepesha bank, inaonekana Diamond Platnumz anawaza kuishi kistaa au kifahari zaidi kama wanavyofanya mastaa wengine wa dunia manake kapost hiyo picha hapo juu kwenye mitandao yake ya kijamii na kisha akaandika haya maneno:

Tuseme Inshallah...#2014 #JusWaitAndSee #KwaniWaoWamewezaje #HadiWeUshindwe #WCB for life Darling......


Sasa tuache mastaa wengine kama Ali Kiba na wengine wapige domo huku Diamond akiuza mdomo.
Diamond Platinumz Akiuza Domo, Waache BongoFleva Wapige Domo Tu! Diamond Platinumz Akiuza Domo, Waache BongoFleva Wapige Domo Tu! Reviewed by Admin on Tuesday, February 04, 2014 Rating: 5

No comments:

Tunapenda kuyasoma maoni/reaction kutoka kwako!

Kama una maoni tofauti na chapisho la hapo juu, wasiliana nasi kupitia ukurasa wetu wa mawasiliano

Powered by Blogger.