Unordered List

Definition List

Salha Israel Akiri Kuzukiwa Na Mapedeshee

MISS Tanzania 2011, Salha Israel ametoboa siri kuhusiana na mapedeshee ambao wamekuwa wakiwapa usumbufu mkubwa kiasi cha kuonekana ni janga la kitaifa kwa warembo
Salha Israel, Miss Tanzania 2011
Akizungumza na Ijumaa kwenye mahojiano maalum hivi karibuni ndani ya ofisi za gazeti hili, Salha alikiri kuwepo kwa watu wenye nia mbaya wanaotumia utajiri wao kujipatia wasichana hali inayosababisha kuichafua Miss Tz.

“Kusema ukweli nilipokuwa kwenye shindano hili sikupata usumbufu sana ila baada ya kupata taji, usumbufu ukaanzia hapo.

“Nikawa napigiwa simu na watu nisiowajua huku wengine wakitaka nionane nao, nimekuwa nikiwakwepa ila ni wasumbufu mno,” alisema Salha aliyekuwa ameongozana na wadogo zake Sabra na Samier.
Salha Israel Akiri Kuzukiwa Na Mapedeshee Salha Israel Akiri Kuzukiwa Na Mapedeshee Reviewed by Admin on Friday, February 14, 2014 Rating: 5

No comments:

Tunapenda kuyasoma maoni/reaction kutoka kwako!

Kama una maoni tofauti na chapisho la hapo juu, wasiliana nasi kupitia ukurasa wetu wa mawasiliano

Powered by Blogger.