Unordered List

Definition List

Snura Awajia Juu BASATA Kwa Kosa La Kumfungia Video Ya Nimevurugwa

Staa wa mziki wa Bongo Snura a.k.a Mamaa Majanga ameamua kukatiza kimya chake baada ya nyimbo yake ya Nimevurugwa kupigwa marufuku nchini Tanzania.

Snura anajitetea kuwa mchezo katika video hio amekuwa akiicheza katika shoo kadhaa na umekubalika. "Mimi na dansa wangu tucheza Nimevurugwa bila wasiwasi wala sijaona mtu yeyote kulalamika." aliongea Snura kwa machungu.

Snura pia ameongezea kuwa kuna video kadhaa ambazo hufanya michezo aina hio na wala haijapigwa marufuku na vituo vyovyote wala BASATA hawajalalamika.

"Imeniuma sana video ya "Nimevurugwa" kufungiwa na BASATA kuonyeshwa kwenye TV bongo wakati kama kukatika ni tamaduni yetu watanzania kuna video kibao za nje za ovyo kabisa wanavaa nusu uchi ila azifungiwi" Snura aliongezea
Snura Awajia Juu BASATA Kwa Kosa La Kumfungia Video Ya Nimevurugwa Snura Awajia Juu BASATA Kwa Kosa La Kumfungia Video Ya Nimevurugwa Reviewed by Admin on Wednesday, February 05, 2014 Rating: 5

No comments:

Tunapenda kuyasoma maoni/reaction kutoka kwako!

Kama una maoni tofauti na chapisho la hapo juu, wasiliana nasi kupitia ukurasa wetu wa mawasiliano

Powered by Blogger.