Unordered List

Definition List

Jokate Atoa Siri Ya Kukutana Na Wema Sepetu

THE big boss wa Kidoti, Jokate Mwegelo ambaye pia ni staa wa sinema na Bongo Fleva, amefichua siri ya kupatana na Wema Isaac Sepetu akisema kuwa sababu ya yeye kuonekana kwenye jukwaa moja na aliyekuwa hasimu wake huyo ni kutafuta amani ya moyo aliyokuwa ameikosa si kweli kwamba alisukumwa na nguvu ya pombe.…

Wawili hao walipatana hivi karibuni wakiwa jijini Arusha.
Akizungumza na gazeti namba moja la burudani Bongo, Ijumaa Wikienda, Jokate alisema ilipokaribia siku ya kwenda Arusha, Wema alimkaribisha kwenye shoo yake iliyofanyika jijini humo lakini alimwambia kuwa amebanwa ila akamuahidi kwamba akimaliza mambo yake atakwenda kumsapoti.

“Wema aliondoka bila kujua kama nitakwenda lakini nilipopanga ratiba yangu ikakaa sawa, niliamua kwenda na kumfanyia ‘sapraizi’ na si kweli kwamba nilisukumwa na nguvu ya pombe,” alisema Jokate.

Jokate alisema kwamba hakushauriwa wala kujadiliana na mtu yeyote isipokuwa aliamua mwenyewe kufanya jambo hilo ambalo lilikuwa likimkosesha faraja kwa muda mrefu.

“Nimeamua kumaliza mabifu kwa sababu nilikosa amani ninayoitaka kwa muda mrefu. Ukweli Wema alinikaribisha, nikaona ndiyo sehemu ya kutimiza lengo langu la kupatana naye,” alisema Jokate ambaye aliingia kwenye gogoro na Wema baada ya kutembea na mpenzi wake, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’.
Global Publishers
Jokate Atoa Siri Ya Kukutana Na Wema Sepetu Jokate Atoa Siri Ya Kukutana Na Wema Sepetu Reviewed by BkuHabari Admin on Monday, February 10, 2014 Rating: 5

No comments:

Tunapenda kuyasoma maoni/reaction kutoka kwako!

Kama una maoni tofauti na chapisho la hapo juu, wasiliana nasi kupitia ukurasa wetu wa mawasiliano

Powered by Blogger.