Unordered List

Definition List

Lulu Atajwa Miongoni Mwa Wanawake Warembo Kumi Afrika

Wasanii hawa ni warembo,wenye kupendeza na watu hupenda sana kufuatilia matukio yao. Wasanii hawa katika nyanja ya filamu wamejikuza na urembo wao ni wakutajika. Kulingana na mtandao wa Swahili World Planet, wameweza kuchambua wanawake warembo kumi ambao wanaongoza kiurembo.
Orodha haijapangwa kimfuatilio.

1. Elizabeth Michael Lulu(18)
Msanii Lulu anapatikana katika filamu za kibongo. Anaamini kuwa yeye ni mrembo ndio maana hutamkuta pahala popote akiwa amevalia wig ama nywele bandia.



 
2.Omotola Jalade(35). 
Mama mwenye watoto wanne ana amebandikwa jina Omosexy, msanii huyu ni maarufu katika filamu za Nigeria, Nollywood. Urembo wake umepita mipaka.


3.Jackie Appiah(29)
Msanii huyu amezaliwa Canada na ameweza kupata umaarufu katika filamu za kighana. Ni mrembo mwenye umbo la kuvutia. Anaonekana katika filamu za Nigeria na Ghana..





4.Jackline Wolper(25)
Msanii huyu wa Kibongo alikiri kuwa yeye hutumia maji na hula majani kwa wingi ili kuhakikisha urembo wake haupotei.. Wolper ni msanii mtajika bongo na amewahi kuonekana katika filamu nyingi mwaka huu.



 5.Genevieve Nnaji(34)
Amebandikwa jina 'Julia Roberts of Africa'. Msanii huyu kwa miaka amehakikisha ametunza urembo wake. Kimsingi ni msanii anayependeza.



6.Nadia Buari(30)
Msanii mwingine wa nchi ya Ghana. Urembo wake ni wa kumezea mate.


7.Yobnesh Yusuph "Batuli"(27)
Mama wa watoto wawili lakini amehakikisha urembo wake uko palepale.

 8.Julieth Ibrahim(27)
Juliet ni msanii mwingine wa Ghana ambaye amekiri kuwa yeye ni mrembo. Katika kuueneza urembo wake, Juliet alisema kuwa yeye ni mrembo zaidi ya mara 100 kumliko Kim Kardashian. Urembo wake ni wakuzaliwa na hakuna upasuaji wowote ama kemikali anazozitumia. Yeye ni mwafrika halisi na anajivunia.
9.Ini Edo(31)
Edo ni mwanamke mrembo zaidi katika Nollywood, urembo wake hauwezi kufichika.


10.Yvonne Cherryl"Monalisa"(32)
Msanii huyu ana watoto wawili lakini jambo hilo halijamzuia Yvonne Cherryl a.k.a Monalisa kujiweka mrembo wakati wote. Ana urembo asili wa kiafrika na yupo katika filamu za kibongo.

Lulu Atajwa Miongoni Mwa Wanawake Warembo Kumi Afrika Lulu Atajwa Miongoni Mwa Wanawake Warembo Kumi Afrika Reviewed by Admin on Monday, November 04, 2013 Rating: 5

1 comment:

Tunapenda kuyasoma maoni/reaction kutoka kwako!

Kama una maoni tofauti na chapisho la hapo juu, wasiliana nasi kupitia ukurasa wetu wa mawasiliano

Powered by Blogger.