Unordered List

Definition List

Penny Amekubali Kugawa Tunda Moja Na Wema,

Peniela Mwingilwa 'Penny’
Mtangazaji wa Kituo cha Televisheni cha DTV, Peniela Mwingilwa ‘Penny’, ambaye ni mpenzi wa mkali wa Bon- go Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ amesema yupo tayari kuchangia map- enzi na msichana mwingine yeyote ambaye atachukuliwa na mwanaume huyo anayem- penda.


Peniela Mwingilwa ‘Penny’.
Penny, chaguo la mama mzazi wa staa huyo wa kibao cha My Number One, amesema maneno hayo, yanayotafsiriwa kama yupo tayari kuchangia mapenzi na hasimu wake, Wema Sepetu ambaye amerejesha uhu- siano wake wa kimapenzi na mwimbaji huyo mpenda vidosho.“Ninampenda Diamond na sitaki kum- poteza. Nia yangu ni kumuona akiwa na furaha.


Kama Diamond anaona kuna msicha- na mwingine wa kutoka naye na kwake hilo linampa furaha, basi mimi sina matatizo kwa sababu ninataka awe na furaha, nitaendelea kuwa naye,” alisema Penny.


Kumekuwa na habari zisizo shaka kwamba Diamond na Wema wamerejesha uhusiano wao na hivi karibuni walitupia picha katika mitandao ya kijamii zilizowaonyesha wawili hao wakiwa katika mapozi ya kimahaba huko Ughaibuni.Ingawa bado Diamond anatoka na Penny, lakini kwa siku za karibuni amekuwa karibu zaidi na mrembo huyo aliyetwaa taji la Miss Tanzania mwaka 2006.
Penny Amekubali Kugawa Tunda Moja Na Wema, Penny Amekubali Kugawa Tunda Moja Na Wema, Reviewed by Admin on Friday, November 08, 2013 Rating: 5

No comments:

Tunapenda kuyasoma maoni/reaction kutoka kwako!

Kama una maoni tofauti na chapisho la hapo juu, wasiliana nasi kupitia ukurasa wetu wa mawasiliano

Powered by Blogger.