Unordered List

Definition List

Daktari Ajipiga Pinafsi Na Joan Rivers Wakati Alipokuwa Amepewa Dawa Za Usingizi

Daktari aliyekuwa akimfanyia upasuaji wa koo Joan Rivers aliacha upasuaji huo kwa muda ili kupiga pinafsi na Joan alipokuwa amepewa dawa za kulala.

Habari hizo za kushangaza zinaeleza kuwa tukio hilo lilifanyika muda mfupi kabla msanii huyo mcheshi kutangazwa kuwa ameingia katoka hali mahututi ya kutojifahamu. Jina la mhudumu aliyekuwa akimfanyia upasuaji limebanwa kwa usalama lakini anaaminika kuwa daktari wa karibu wa staa huyo.

Mmoja wa wafanyikazi katika kliniki hio ya Manhattan’s Yorkville Endoscopy aliiambia CNN kuwa jamaa huyo aliyekuwa akimfanyia upasuaji Rivers alikuwa mtu mwenye utata na hakuwa ana vyeti tajika katika shughli nzima ya upasuaji.

Joan alikuwa na matatizo ya sauti ya koo na alikuwa afanyiwe utaratibu wa kawaida wa kutengeneza sehemu yake ya koo kabla kukumbana na mshtuko wa moyo mwezi August 29.
Daktari Ajipiga Pinafsi Na Joan Rivers Wakati Alipokuwa Amepewa Dawa Za Usingizi Daktari Ajipiga Pinafsi Na Joan Rivers Wakati Alipokuwa Amepewa Dawa Za Usingizi Reviewed by Admin on Wednesday, September 17, 2014 Rating: 5

No comments:

Tunapenda kuyasoma maoni/reaction kutoka kwako!

Kama una maoni tofauti na chapisho la hapo juu, wasiliana nasi kupitia ukurasa wetu wa mawasiliano

Powered by Blogger.