Unordered List

Definition List

Kanye West Ana Masharti Ya Nyumbani Ya Kukwaza, Jarida La Uingereza Lafichua

Kama ingewezekana Kanye West angetamani kuitwa mungu mdogo, kando na kuwa tayari ana wafuasi wanaomwita kuwa yeye ndiye Yeezus.
Wikendi iliopita nchini Australia Kanye West alizua utata baada ya kulazimisha walemavu wawili wasimame ndipo aendeleze shoo, na sasa jarida moja la Uingereza linadai kuwa Kanye West nyumbani kwake New York ana masharti magumu yasioeleweka vyanzo vyake.

Kulingana na mwandani wa Kanye anadai kuwa Kanye akiwa kwa nyumba yake iliopo New York basi viwango vya joto nyumbani humo lazima viwekwe kadri ili aweze kuvaa nguo za magauni zenye kumfunika hadi kichwa aka hood.

Sharti jingine ni kuwa maid mmoja tu ndiye anayeruhusiwa chumbani mwa kulala mwa Kanye na anafaa kufanyiwa uchunguzi kabla kuingia. Nguo za Kanye za kuoshwa hazifai kushikwa na mtu mwingine ila maid huyo mmoja pekee.

Nyingine ni kuwa Kanye haruhusu mgeni yeyote ashike simu akiwa mbele yake, pia Kanye anadaiwa kusikiliza nyimbo kwa sauti ambayo lazima iwe kiwango flani wakati wowote ule.

Halafu waambiwa hiki ni kionjo tu cha maisha ya Kanye West, na kama kweli tungetaka kujua siri za staa huyu basi ingekuwa bora kama kungekuwa na kipindi kiitwacho Keeping Up With Yeezus, bila hivyo hatuwezi kujua mengi ya Kanye.
Kanye West Ana Masharti Ya Nyumbani Ya Kukwaza, Jarida La Uingereza Lafichua Kanye West Ana Masharti Ya Nyumbani Ya Kukwaza, Jarida La Uingereza Lafichua Reviewed by Admin on Wednesday, September 17, 2014 Rating: 5

No comments:

Tunapenda kuyasoma maoni/reaction kutoka kwako!

Kama una maoni tofauti na chapisho la hapo juu, wasiliana nasi kupitia ukurasa wetu wa mawasiliano

Powered by Blogger.