Unordered List

Definition List

LUCY KOMBA AMSHANGAA AUNT KUISHI MBALI NA MUMEWE

MWANADADA anayefanya poa kwenye anga la filamu Bongo, Lucy Komba amejikuta akibaki na viulizo vingi kutokana na kitendo cha msanii mwenzake, Aunt Ezekiel kuishi mbali na mumewe anayefahamika kwa jina la Demonte kwa kipindi kirefu, jambo ambalo yeye hawezi kulifanya.

Akizungumza na paparazi, msanii huyo alisema kitendo cha Aunt kuolewa na kuishi mbali na mumewe kinamfanya abaki na maswali mengi kichwani, sababu wanandoa kuishi mbalimbali husababisha wahusika kuumizana kichwa kwa kiasi kikubwa na kukosa amani ya moyo.

“Namshangaa Aunt anawezaje kuishi mbali na mumewe kwa kipindi kirefu, binafsi siwezi. Kama hivi ninavyotarajia kuolewa hivi karibuni, nimekubali kuachana na dili zangu zote za hapa Bongo, nikiolewa naenda kuishi Denmark kwa mume wangu,” alisema Lucy Komba.
-GPL
LUCY KOMBA AMSHANGAA AUNT KUISHI MBALI NA MUMEWE LUCY KOMBA AMSHANGAA AUNT KUISHI MBALI NA MUMEWE Reviewed by Admin on Monday, September 01, 2014 Rating: 5

No comments:

Tunapenda kuyasoma maoni/reaction kutoka kwako!

Kama una maoni tofauti na chapisho la hapo juu, wasiliana nasi kupitia ukurasa wetu wa mawasiliano

Powered by Blogger.