Unordered List

Definition List

Hussein Machozi Afunguka Kuhusu Issue Ya Fumanizi Na Mke Wa Mwanasiasa

Star wa bongo Hussein Machozi hatimaye amezungumzia tukio lililotokea mwezi uliopita na kupelekea vyombo vingi vya habari nchini Kenya kuripoti kuwa amekamatwa akizini na mke wa mwanasiasa maarufu mjini Mombasa.

Haya ndio maelezo ya hit maker wa ‘Kwa ajili Yako’ kuhusu kilichotokea, alipozungumza na Millard Ayo kupitia Amplifaya ya Clouds FM (Agosti 28).

“Ukweli ni kwamba hiyo story imekuzwa yaani imekuwa kubwa sana tofauti na jinsi mambo yalivyokuwa. Kama masaa 24 nilipewa sasa mbona bado nipo Kenya…Ile ishu ilikuwa hivi, tulikuwa tumekwenda kuingia deal hotelini kama tunavyokutanaga, sasa Yule mtu aliyekuwa ananipa deal alikuwa yupo pale hotelini akaniita twende tukaongee kupanga mikakati na kila kitu, lakini baadae kumbe alikuwa na beef sijui na mume wake au sio bana, kwa hiyo mume wake alikuja pale kuanza kumletea fujo lakini mimi sikuwa kwenye uhusiano wowote, watu wakaleta fujo pale na nini mimi mbona nikaondoka fresh tu lakini hamna lolote ni kwamba tulikuwa tumekaa nae tunaongea mchakato wa biashara…hotelini kama maeneo ya kupumzika hivi kama sehemuya mikutano hivi”.
Hussein Machozi Afunguka Kuhusu Issue Ya Fumanizi Na Mke Wa Mwanasiasa Hussein Machozi Afunguka Kuhusu Issue Ya Fumanizi Na Mke Wa Mwanasiasa Reviewed by Admin on Monday, September 01, 2014 Rating: 5

No comments:

Tunapenda kuyasoma maoni/reaction kutoka kwako!

Kama una maoni tofauti na chapisho la hapo juu, wasiliana nasi kupitia ukurasa wetu wa mawasiliano

Powered by Blogger.