Unordered List

Definition List

Martin Kadinda Adai Kuwa Wema Sepetu Hana Pesa Za Kummudu

Martin Kadinda ambaye ni meneja wa Wema Sepetu ameibuka na kusema kuwa Wema Sepetu aliyekuwa akimwaga pesa vilivyo kwa sasa hana pesa ya kumlipa bali yeye Martin anahangaika kwa issue zake binafsi ili wasilale njaa…

Kadinda amesema kuwa yeye na Wema hawana mkataba wa kulipana bali wapo kishkaji zaidi.“Wema hana pesa ya kunilipa mimi, ninachokifanya ni kuhangaika kutafuta deals ili mimi na yeye maishani tusilale njaa, maisha ni kutegemeana. “Kikubwa ninachofanya ni kutafuta dili za kazi nyingi ili tuweze kupeana pasu kwa pasu lakini si mshahara, nafanya kazi na bosi wangu Wema kishikaji na kwa kweli nafurahia sana utaratibu huu”

Martin alisema kuwa kama angekuwa na mkataba na Wema kumlipa kila mwezi asingemudu na kusema yupo na Wema kwa sababu anajua ni mtu wa aina gani na anafanya kazi zake kwa uhuru bila kubanwa.

Wakati Wema yupo kimapenzi na yule kigogo aliyejulikana kwa jina la Clement(CK), Wema alidaiwa kumwaga pesa kila kona na wapambe kibao wa kula bata nao huku akiwa na magari kadhaa lakini kwa sasa anadaiwa kushuka kiuchumi na kubaki na gari moja pekee huku wapambe aliokuwa nao wakitimua na waliobaki kulalamika hawali bata kama zamani.

Hivi karibuni tena Diamond Platnumz aliyempenzi wa Wema alisema kuwa Wema ni mtu wa starehe na kuendekeza mashoga wapenda anasa badala ya kutumia fursa na umaarufu mkubwa alionao sasa kufanya kazi zake kwa bidii hususani filamu.
Martin Kadinda Adai Kuwa Wema Sepetu Hana Pesa Za Kummudu Martin Kadinda Adai Kuwa Wema Sepetu Hana Pesa Za Kummudu Reviewed by Admin on Tuesday, September 02, 2014 Rating: 5

No comments:

Tunapenda kuyasoma maoni/reaction kutoka kwako!

Kama una maoni tofauti na chapisho la hapo juu, wasiliana nasi kupitia ukurasa wetu wa mawasiliano

Powered by Blogger.