Unordered List

Definition List

Ray C Amuokoa Mrembo wa Video ya Ice Cream Baada ya Kuzidiwa na Madawa ya Kulevya

Story na Udaku
Unaikumbuka nyimbo ya Ice Cream iliyoimbwa na Noorah? Ni nyimbo nzuri iliyotamba miaka iliyopita na kuvuma zaidi baada ya video yake kutoka ambapo ndani yake kulikuwa na Video queen aliyefahamika kwa jina la Doreen.

Taarifa zilianza kusambaa kuwa mwanadadahuyo kwa sasa ametumbukia katika tatizo lamatumizi ya dawa za kulevya huku akihitaji msaada mkubwa.

Kupita ukurasa wa Instagram mwanamuziki Ray C ambaye nae aliwahi kukumbwa na tatizo hilo akiweka picha yake pamoja na Doreen huku akidai kuwa amempata na amekubali kuanza matibabu kuachana na dawa za kulevya.

Ray C ameandika kupitia Instagram >>> ‘Mungu ni mwema sana!!tena sana!!nilipotangaza kuwa nimefungua taasisiyangu ya kuelimisha jamii kuhusu athari za dawa za kulevya nilipata emails nyingi kuhusu kumsaidia Doreen video queen aliecheza kwenye video ya Noorah iitwayo ice cream!!
Nilijaribu kumtafuta baada ya kuona picha yake kwenye website ya vibe magazine ’‘Roho iliniuma sana nikamwomba Mungu anisaidie nimpate!! namshukuru Mungu asubuhi ya juzi nikiwa ofisini nikaona email kutoka kwa dada yake Doreen kichwa cha habari kikiwa msaada, nilipoisoma chozi lilinitoka nika reply mara moja nilimuombaanitumie namba yake tuongee nikampigia akaniambia doren hali yake si nzuri kutokana na drugs

’‘Moyoni nikawa nafikiria huyu dada angejua jinsi nilivyomtafuta mdogo wake !!!!! ikawa Kama bahati tukaongea kwa kirefu sana na nikamwambia tukutane kitengo cha dawa Mwananyamala! nilipomuona Doren kwa mara ya kwanza nilifurahi kupita maelezo ila nikawa na wasiwasi kuhusu utayari wake wa kuanza tiba ya methadone, isije ikawa amelazimishwa kuja akaniambia dada yangunimechoka maisha ya utumwa nisaidie!!

’‘Hicho ndo nilichotaka kusikia nikamwambiakwa uwezo wa Mungu Shetani ameshindwa!!!!!! am soooo happy Doren ameanza tiba ya Methadone!!! wapenzi wotewa bongoflava nawaomba tumwombee mdogo wetu aweze kusimama kwenye tiba na ashinde majaribu ya Shetani na aishi kwaamani bila utumwa wa shetani

’‘God We Trust!!!I love You my lil’ sister….. nawahamasisha wengine huko mliko mwenye ndugu, jamaa au rafiki njoo katika taasisi yetu uweze kusaidiwa! usikubali maisha ya utumwa wa dawa za kulevya, njoo tukusaidie… Ray C Foundation pamoja na kitengo cha Methadone We love you guys, We can help you….”

Ray C Amuokoa Mrembo wa Video ya Ice Cream Baada ya Kuzidiwa na Madawa ya Kulevya Ray C Amuokoa Mrembo wa Video ya Ice Cream Baada ya Kuzidiwa na Madawa ya Kulevya Reviewed by Admin on Tuesday, May 27, 2014 Rating: 5

No comments:

Tunapenda kuyasoma maoni/reaction kutoka kwako!

Kama una maoni tofauti na chapisho la hapo juu, wasiliana nasi kupitia ukurasa wetu wa mawasiliano

Powered by Blogger.