Unordered List

Definition List

BONGO MOVIE WAITAKASA NDOA YA RAY NA CHUCHU HANS

Ray na Chuchu katika pozi la kimahaba


BAADA ya kuzagaa kwa fununu za chini ya kapeti kuwa mastaa wa sinema za Kibongo, Vincent Kigosi na Chuchu Hans kutarajia kufunga ndoa, wenzao wa Bongo Movie wameonesha hadharani kuwa wanaiunga mkono ndoa hiyo na kutoa baraka zao. Tukio hilo lilijidhihirisha wazi hivi karibuni katika Viwanja vya Leaders Club, Kinondoni jijini Dar katika uchaguzi wa viongozi wa Klabu ya Bongo Movie ambapo Ray ambaye alikuwa mwenyekiti mstaafu wa klabu hiyo, aliambatana na ‘bebi’ wake huyo (Chuchu) na kupozi katika staili ya ‘mista na misezi’.

Bila kupepesa macho, kwa nyakati tofauti mastaa hao waliokuwa wakifuatilia uchaguzi huo, wa kiume walimuita Chuchu shemeji huku wa kike wakimuita Chuchu wifi ambapo bibie aliitikia bila hiyana.

“Tunajua kuwa Ray na Chuchu ni wapenzi na tuko tayari kushuhudia ndoa yao na tutatoa mchango wowote utakaohitajika kwa ajili ya kufanikisha harusi yao kwani wanaonekana kupendana, tangu nianze kuona uhusiano wa wasanii hakuna hata mmoja aliyewahi kuwa na mapenzi ya dhati kama wanayoonesha Ray na Chuchu,” alisema mmoja wa wasanii aliyeomba hifadhi ya jina.

Staa mwingine mwenye ‘taito’ kubwa ndani ya Bongo Movies, kwa sharti la kutotaja jina lake alisikika akisema: “Ray na Chuchu wanaonyesha penzi lisilo na unafiki hata chembe, kama ilivyozoeleka kwa wasanii wengine na ndiyo maana leo utaona wanaenda sehemu zote wakiwa pamoja na wala hawajifichi kwa lolote lile.”

Kuonesha kuwa wanapendana, Chuchu alionekana kumrekebisha nguo vizuri Ray kila alipogundua imekaa vibaya huku wakichagiza ‘malovee’ yao kwa ‘hagi’ na kukumbatiana kwa kishkaji.
BONGO MOVIE WAITAKASA NDOA YA RAY NA CHUCHU HANS BONGO MOVIE WAITAKASA NDOA YA RAY NA CHUCHU HANS Reviewed by Admin on Saturday, January 11, 2014 Rating: 5

No comments:

Tunapenda kuyasoma maoni/reaction kutoka kwako!

Kama una maoni tofauti na chapisho la hapo juu, wasiliana nasi kupitia ukurasa wetu wa mawasiliano

Powered by Blogger.