Unordered List

Definition List

Loliondo Kwa Babu Kumezuka Mapya

Nimeambiwa kuwa kwa sasa kuna watu wa nguvu kibao wanaenda Samunge, Loliondo na kinachowapeleka sio ishu ya Kikombe cha babu tena sasa hivi ni madini ya dhahabu ambayo inasemekana yamegundulika eneo hilo.

Taarifa kutoka kijijini hapo zinasema kuwa watu wanaongezeka kijijini hapo kwa ajili ya kujipatia madini hayo yanayosemekana yapo katika mashamba ya watu na maeneo ya kingo za Mto katika Kijiji cha Mgongo kilichopo jirani na kwa Babu.

Kwa babu zamani za kale
Diwani wa Samunge Jackson Sandea amesema kwa sasa kuna zaidi ya watu 4,000 na bado wanaongezeka na kusema kuwa idadi hiyo ya watu inaweza kuwa zaidi ya kikombe cha babu kwa kipindi kile.

Ingawa eneo rasmi zaidi bado halijatjwa ila inasemakana mbali na kupatikana kwenye mto huo pia dhahabu hiyo ianapatikana hata kwenye mashamba ya watu,kwa sasa Kamishna wa Madini Kanda ya Kaskazini Alex Magayane amesema wanajiandaa kwenda kijijini hapo baada ya kupokea taarifa za kugundulika kwa dhahabu kwenye eneo la Samunge.

Imeandikwa na gazeti la Mwananchi.
Loliondo Kwa Babu Kumezuka Mapya Loliondo Kwa Babu Kumezuka Mapya Reviewed by BkuHabari Admin on Wednesday, May 21, 2014 Rating: 5

No comments:

Tunapenda kuyasoma maoni/reaction kutoka kwako!

Kama una maoni tofauti na chapisho la hapo juu, wasiliana nasi kupitia ukurasa wetu wa mawasiliano

Powered by Blogger.