Wana
mashabiki wengi, miongoni mwao tayari ni mamilionea (wa shilingi), wapo
wenye mijengo, magari ya kifahari, miradi ya biashara, makampuni,
endorsements na vitu vingine. Hawa ndio wasanii 12 wa Tanzania wenye
nguvu zaidi mwaka 2014.
Diamond Platnumz
Diamond
Platnumz ndiye msanii anayeandikwa zaidi kwenye vyombo vya habari
Afrika Mashariki kwa sasa. Hadi sasa Diamond amefikia hatua ambayo
haijawahi kufikiwa na msanii yeyote wa Tanzania. Ndiye msanii mwenye
show nyingi zaidi kwa sasa.
Kimataifa
2014 umekuwa wa mafanikio zaidi kwake kuanzia kutajwa kuwania vipengele
viwili kwenye tuzo za MTV MAMA, BET Awards, kushiriki kwenye wimbo
uliokutanisha mastaa takriban 20 wa kampeni ya ‘Do Agric’ ‘Cocoa na
Chocolate, pamoja na wimbo ‘Africa Rising’ uliomkutanisha na wasanii
kama Mi Casa Music, Davido, Sarkodie na Tiwa Savage.
Diamond akihojiwa na Karrueche Tran kwenye red carpet ya BET Awards, June 29, 2014
Pia
pamoja na kufanya wimbo na Davido, Diamond ameshafanya collabo na
wasanii wengine wa Nigeria wakiwemo Iyanya, Waje na Dr Sid pia hivi
karibuni ameshirikishwa na kundi la Afrika Kusini, Mafikizolo.
Diamond na Wema kwenye red carpet ya MTV MAMA 2014, Durban, SA
Pamoja
na kukosa tuzo za kimataifa alizotajwa kuwania, staa huyo mwaka huu
alivunja rekodi kwa kuchukua tuzo zote saba alizotajwa kwenye KTMA na
pia kushinda tuzo za watu zilizotolewa June 27.
Akiwa
na video mbili mpya kibindoni, moja ya wimbo aliofanya na Iyanya na ile
ya wimbo wake ‘Mdogo Mdogo’, Diamond ana uhakika wa kuendelea kuutawala
mwaka 2014.
Lady Jaydee
Judith
Mbibo aka Lady Jaydee ndiye msanii wa kwanza wa Tanzania kufikisha
likes 300,000 kwenye mtandao wa Facebook huku sasa idadi ikiwa ni zaidi
ya 329,000. Tangia June mwaka jana alipofanya show yake ya miaka 13 ya
muziki wake na kuijaza Nyumba Lounge watu wasipate pa kukanyaga, Lady
Jaydee haoneshi dalili za kusimama. Baada tu ya kutoka kwenye Coke
Studio Africa, Jaydee alishiriki kwenye wimbo maalum kwaajili ya kombe
la dunia wa Coca Cola, ‘The World is Ours’. Pamoja na show zisizo
katika, biashara yake kuu ya mgahawa imeendelea kufanikiwa.
Kwa
mujibu wa meneja wake, Gadner G Habash ambaye pia ni mumewe pamoja na
kuwa na biashara yake ya Nyumbani Lounge, Lady Jaydee anatarajia
kuongeza zaidi miradi mingine. “Huyu bado ni mjasiriamali mchanga
anayejifunza zaidi na angependa kufanya biashara nyingi lakini muda ni
mdogo. Isipokuwa kwa mwaka huu alitarajia kufanya kitu kingine kuongeza
kama biashara. Hajawa tayari kusema ni kitu gani lakini mwenyezi Mungu
akijaalia heri na afya mwaka huu kuna biashara nyingine Jaydee
ataitambulisha, ukiacha Nyumbani Lounge na muziki,” Gadner aliiambia
Bongo5 kwenye mahojiano maalum.
Mwaka
huu Jide alipata pia endorsement kutoka kwenye kampuni ya vipodozi ya
Sweden Oriflame Cosmetics na kuungana na wanawake wengine watatu maarufu
wa Afrika Mashariki kuwa mabalozi wa bidhaa zao katika nchi zao. “Lady
Jaydee, Juliana and Jamila have been named because their style and
approach to beauty is the ideal representation for the Oriflame brand.
They are strong and talented women who many people across East Africa
readily identify with,”alisema mkurugenzi mtendaji wa kampuni hiyo
Afrika Mashariki Mr. Klas Kronaas wakati akiwatangaza.
June
28, Lady Jaydee alikuwa mmoja wa wasanii waliotumbuiza kwenye tukio la
Masaku Rugby 7s After Party lililofanyika huko Machakos Kenya. Takriban
watu 40,000 walihudhuria kwenye show hiyo iliyodhaminiwa na Tusker
Lager. Wasanii wengine walitumbuiza ni pamoja na Jua Cali, Radio n
Weasel, Wyre, Kidum, Keni wa Maria.
Kingine ni kubwa ni kuwa Lady Jaydee ataungana na Ali Kiba kutoka Tanzania kupanda jukwaa moja na Nicki Minaj, J Cole na wasanii wengine wa Marekani na Afrika kwenye tamasha la TribeOne Dinokeng litakalofanyika September mwaka huu nchini Afrika Kusini.
Kingine ni kubwa ni kuwa Lady Jaydee ataungana na Ali Kiba kutoka Tanzania kupanda jukwaa moja na Nicki Minaj, J Cole na wasanii wengine wa Marekani na Afrika kwenye tamasha la TribeOne Dinokeng litakalofanyika September mwaka huu nchini Afrika Kusini.
AY
Kimuziki
mwaka 2014, AY ameendelea kufanya movements nyingi ikiwa ni pamoja na
kuachia wimbo wake ‘Asante’. Akiwa amebobea zaidi katika shughuli za
ujasiriamali, mwaka 2014 umekuwa mzuri kibiashara kwake kutokana na
kupata endorsement kuwa ikiwemo ile ya kampuni ya Samsung. Pia aliungana
na Diamond kwenye mradi wa ‘Do Agric’ wa One Campaign.
Hivi
karibuni pia, AY ambaye jina lake halisi ni Ambwene Yessaya pamoja na
aliyewahi kuwa Miss Tanzania, Faraja Kotta Nyalandu, waliteuliwa kuwa
mabalozi wa UNICEF Tanzania katika mradi wa kupiga vita ukatili kwa
watoto.
Akiwa mmoja wa waanzilishi wa kipindi cha TV kilichoshinda tuzo za watu, Mkasi, AY ana mpango wa kukivukisha boda.
Kwa mujibu wa mtandao wa Nairobi Wire, mwaka huu AY alienda Kenya na crew ya Mkasi inayomjumuisha mtangazaji Salama Jabir na Josh Murunga, kwa ajili ya kuangalia fursa zinazoweza kupatikana nchini humo kwa lengo la kutaka kupanua wigo wa kipindi hicho. “Tuko hapa kwanza kuangalia uwezekano wa kupanua biashara ya kipindi chetu” alisema AY.
Kwa mujibu wa mtandao wa Nairobi Wire, mwaka huu AY alienda Kenya na crew ya Mkasi inayomjumuisha mtangazaji Salama Jabir na Josh Murunga, kwa ajili ya kuangalia fursa zinazoweza kupatikana nchini humo kwa lengo la kutaka kupanua wigo wa kipindi hicho. “Tuko hapa kwanza kuangalia uwezekano wa kupanua biashara ya kipindi chetu” alisema AY.
Hata hivyo, kuna mambo mengi makubwa yanayoendelea katika himaya ya rapper huyo ambayo bado hajayaweka hadharani.
Nay wa Mitego
Nay
wa Mitego ni rapper anayeendelea kuwashangaza wengi kwa mafanikio yake
makubwa kimuziki na maisha yake binafsi. Rapper huyo ameendelea kuwa
miongoni mwa rappers wa Tanzania wenye mashabiki wengi nchini huku
nyimbo zake zikiwa na ushawishi mkubwa. Hivi karibuni, aliungana na
Vanessa Mdee na Barnaba kama mabalozi wa kampeni ya Switch On ya Airtel.
Aliwashangaza
watu wengi zaidi baada ya kuonesha nyumba yake ya kifahari aliyoijenga
kwa takriban shilingi milioni 150 huku pia akimiliki magari ya bei.
“Gari
yangu mpya Nissan Murano nimenunua milioni 36, ni gari ambayo naipenda
sana ,dream car yangu kwenye maisha yangu ni Murano , ninaweza
nikabadilisha nikawa na gari nyingine, pia mimi napenda nyumba nzuri
,napenda kuishi kwenye nyumba nzuri, nina nyumba tatu, hii hapa ambayo
nahamia kesho ina thamani ya shilingi milioni 170 kila kitu, lakini
inaweza ikawa zaidi ya milioni 170 kwasababu kuna vitu vingine huwa
sivipigii hesabu,” Nay aliiambia Bongo5.
Vanessa Mdee
Vanessa
Mdee aliwahi kuiambia Bongo5 kuwa mafanikio aliyoyapata sasa hakuwahi
kuyafikiria. “Nilikuwa natarajiwa makubwa lakini haya ni makubwa haswaa.
Ukiwa unafanya kazi ya muziki you hope for things to work out, you hope
for things to be beneficial. Kwahiyo naona kama taratibu muziki wa
Tanzania umebadilika na wasanii wameanza kupewa kipaumbele so I am just
happy to do what I love to do,” alisema.
Mafanikio
hayo ni pamoja na kushinda tuzo ya KTMA, kushiriki kwenye tour, kufanya
matangazo ya biashara, kuchaguliwa kushiriki msimu wa pili wa Coke
Studio Africa, kuhusishwa kwenye kipindi cha Introducing cha Channel O
na mengine. Pamoja na kuwepo watu waliokuwa na mashaka na kipaji chake,
Vee Money ameendelea kuwashangaza wengi na kujikusanyia mashabiki wa
kila aina.
“Mpaka
leo wapo wenye mashaka na mimi. Hainikatishi tamaa bali inanipa
changamoto kuendelea kuwaprove wrong na kuendelea kufanya kitu kizuri
mpaka wale waliokuwa na mashaka na mimi wakubali waseme ‘yeah she is the
one’. So I don’t mind a few doubters,” anasema.
Ommy Dimpoz
Mwaka
huu, Ommy Dimpoz ni miongoni mwa wasanii waliofanya show nyingi za nje
kwa ziara ya Ulaya, Marekani na Asia. Pia amekuwa amekifanya show nyingi
za nyumbani zinazomuingizia fedha nyingi. Diamond, amewahi kumtaja Ommy
kama msanii anayefuata nyayo za mafanikio yake. Hili limedhihirika
baada ya kuachia video ya wimbo wake ‘Ndagushima’ iliyoongozwa na Moe
Musa.
Ommy
Dimpoz aliiambia Bongo5 kuwa amepata jibu la kwanini kuwekeza na
kufanya video nzuri kuna faida kubwa. Alisema hakutegemea kuwa kuna siku
video yake itakuwa ikichezwa kama kawaida kwenye vituo vikubwa vya TV
barani Afrika.”Kupigwa video kwenye channel kubwa sio tatizo, video
nyingi sasa hivi zinaenda lakini unawashawishi vipi wakupe pia rotation?
Ni Uzuri wa video, pengine wanaangalia director amefanya nani,”
alisema.
Mwaka 2014, Ommy ameandaa show nyingi zake mwenyewe bila kutegemea promoter na hivyo kuingiza fedha nyingi zaidi na pia kumsaidia kuwa miongoni mwa wasanii wanaochaji fedha nyingi kutumbuiza.
Mwana FA
Hamis
Mwinjuma aka Mwana FA ni msanii anayeongoza kwa kuyafanya mashairi ya
nyimbo zake kugeuka sentensi kwenye midomo ya watu wengi. Mwaka huu
wimbo wake ‘Mfalme’ umeongelewa zaidi mitandaoni na kuupa heshima ya hit
isiyohitaji maswali.
FA
ameendelea kuwa mchawi wa steji na mara nyingi yeye na AY wameendelea
kuwa miongoni mwa rappers wakali jukwaani. Shughuli nyingi binafsi
anazofanya Mwana FA zimeendelea chini ya kapeti lakini kuna mambo
makubwa anayoyafanya.
Profesa J
Mwaka
2014, Mchawi wa Rhymes, Profesa Jay amerejea tena kwenye chart kwa
ngoma yake ‘Kipi Sijaskia’ aliyomshirikisha, Diamond. Profesa ameendelea
kujiimarisha kwenye miradi mbalimbali ya biashara ikiwa ni pamoja na
kufungua studio yake ‘Mwanalizombe Recs’.
Pamoja
na muziki, mwaka huu Profesa aliteuliwa kuwa mmoja wa mabalozi wa
taasisi ya kilimo isiyo ya kiserikali (Ansaf) ambao hivi karibuni akiwa
na AY walimkabidhi Rais Kikwete taarifa ya maoni kutoka kwa wakulima wa
Tanzania, katika mkutano wa maswala ya kilimo uliyofanyika ndani ya
hotel ya Double Tree.
Joh Makini & Nick wa Pili
Kwa
mwaka 2014, Joh na mdogo wake Nick wamekuwa wakifanya mambo mengi ya
muziki pamoja. Mwaka huu Weusi wamekuwa rappers wa Tanzania wenye video
kali zaidi kuliko wote na zilizofika mbali. Walianza na ile iliyoongozwa
na mshindi wa tuzo za watu, Nisher ya wimbo wao ‘Nje ya Box’
iliyoandika historia kwa kuwa video yao ya kwanza kuchezwa Channel O.
Hawakusubiri kwa muda mrefu kwa kuachia video nyingine waliyoshoot Kenya
ya ngoma yao ‘Gere’.
Pamoja
na ngoma za Weusi, ndugu hawa wameendelea kushambulia kwa ngoma zao
binafsi ambapo Nick aliachia wimbo ‘Staki Kazi’ uliopata shavu bungeni.
Naye Joh Makini hivi karibuni aliachia single yake ‘Najiona Mimi’ aka I
See Me’ iliyoendelea kumthibitisha kuwa mchawi wa hip hop. Weusi
wameendelea kujimaarisha katika biashara zao kwa kuingiza sokoni bidhaa
mbalimbali zikiwemo masweta, kofia, miwani na bidhaa zingine.
Fid Q
Fareed
Kubanda aka Fid Q ameendelea kuwa rapper mwenye ushawishi mkubwa si tu
kwa mashabiki wa hip hop, bali pia rappers wenzie. Uwezo wake wa
kufikiri, maarifa anayoyapata kutokana na desturi yake ya usomaji wa
vitabu, vimemfanya aendelee kuwa rapper mwenye mashairi makali zaidi
Tanzania.
Pamoja
na muziki, Fid ameendelea kujihusisha na shughuli za kijamii ikiwa
pamoja na kusimamia vijana wa Hip Hop Darasa na pia kujihusisha na
utengenezaji wa filamu za makala kuhusu masuala ya kijamii. Moja ya
filamu aliyoshiriki kwa kusimulia ilioneshwa kwenye tamasha la ZIFF 2014
lililomalizika hivi karibuni.
Feza Kessy
Feza
Kessy ana bahati ya kuwa msanii wa Tanzania mwenye mashabiki waaminifu
nje ya nchi anayotokea. Uhusiano wake na mshiriki wa Big Brother Africa
2013, Oneal wa Botswana, umemfanya atengeneze kundi la mashabiki
lijiitalo ‘Ninjas’ ambalo lipo nyuma yake katika shida na raha. Akiwa
masomoni nchini Afrika Kusini, Feza ameendelea kufuata ndoto yake ya
kuwa mwanamuziki mkubwa Afrika.
“Kunakuwa
kuna shule, halafu kunakuwa na appearance job nafanya, just to appear
as Feza Kessy , kuchukua picha na mashabiki na vitu kama hivyo. Pia
sometimes nakuwa nafanya shows lakini sanasana inakuwa ni Botswana,”
aliiambia Bongo5. Hivi karibuni, alishoot video ya wimbo wake mpya ‘My
Papa’ na inatarajiwa kutoka hivi karibuni
Source BONGO5.COM
Source BONGO5.COM
Hawa Ndio Wasanii Wenye Nguvu Zaidi Tanzania 2014 Kulingana Na Bongo5
Reviewed by BkuHabari Admin
on
Thursday, July 03, 2014
Rating:
No comments:
Tunapenda kuyasoma maoni/reaction kutoka kwako!
Kama una maoni tofauti na chapisho la hapo juu, wasiliana nasi kupitia ukurasa wetu wa mawasiliano