Wakati wanawake wengine wakionekana kubembeleza penzi na kujinyenyekeza kwa wapenzi wao ili wasiachike, Lulu Michael anasema hana muda huo kwani uzuri wake unatosha kuwavuta wanaume wa kila aina kutoka katika kila kona ya Tanzania.....
Lulu amedai kuwa inawezekana mwanaume wa kwanza kwake ndo chaguo lake namba moja, lakini suala la kuanza kulilia mapenzi au kuumia halipo na kamwe hawezi kufanya hivyo.
"Mapenzi ni magumu hasa kwetu sisi wasanii. Kuna wanaume wanaweza kuja kwako ukadhani ni wema lakini baada ya kumaliza haja zao huwaoni, ndo maana huwa sioni haja ya kujilizaliza kwa mwanaume coz akigundua umezimika ndo kabisa atakugeuza Toilet paper ya kuchambia......
"Najua wapo wengi sana wanaonitamani, lakini kwa taarifa yao ni kwamba nipo makini sana na naitambua thamani yangu." Alisema Lulu.
Hata hivyo Lulu alisema kuwa huwa anatongozwa na wanaume wengi sana kutokana na uzuri alionao, hali inayomfanya abadilinamba ya simu kila mara kukwepa usumbufu.
Lulu Michael Agusia Kuhusu Mapenzi
Reviewed by Admin
on
Sunday, June 29, 2014
Rating:
No comments:
Tunapenda kuyasoma maoni/reaction kutoka kwako!
Kama una maoni tofauti na chapisho la hapo juu, wasiliana nasi kupitia ukurasa wetu wa mawasiliano