Unordered List

Definition List

Dalili 10 Za Kuonyesha Kuwa Yule Mwanamume Anakutongoza (Wanawake)


Ushawahi kujiuliza kama yule mwanamume unayekutana naye kila siku anakutongoza? Kuna njia kadhaa ambazo zimefanyiwa utafiti ambazo zitakushangaza. Ijapokuwa ni vigumu kutambua kama anakutongoza kupitia maneno ya kimwili (body language), unaweza kujua pale anapoanza.
Hizi hapa ndizo dalili 10 ambazo wanaume hufanya wakiwa wakijitambua au bila kujitambua kukuonyesha kuwa wamekupenda.

1. Tabasamu la upendo
Tabasamu ni njia rahisi ya kuonyesha kama mtu anakupenda haswa ikija maswala ya kutongoza. Ukimwona mwanamume anakurushia tabasamu la upendo kila wakati basi ufahamu kuwa umempendeza na anatafuta njia ya kukupata. Labda anashikwa na haya ya kukutongoza so kama mwanamke nafasi hio usiitupe, itumie vizuri ipasavyo. Akismile pia nawe umrudishie, zaidi waweza kuanzisha maongezi.

2. Kushikwa na haya wa kuongea (shy blush)
Nafahamu waelewa ni vigumu kufanya maongezi/kutongoza na wanaume wenye haya, lakini hio haimaanishi kuwa wanawake waache kabisa kujihusisha na watu kama hawa. Ukiona kama mwanamume anashindwa kabisa kustahimili kuwa mbele yako (kushikwa na haya) hii ufahamu ni dalili kuu kuwa anakutongoza. Lakini pia fahamu kwamba si wanaume wenye haya pekee ndio huweza kubabaika mbele yako bali naturally kwa mwanamume yeyote. Kwa kawaida jambo hili huwa hujitokeza bila kujizuia...na likijitokeza fahamu kuwa amekutaka.

3. Kukuangalia kwa macho
Swala hili laweza kuwa na tashwishi kiasi lakini pia ni vyema kuliangalia kwa umakini. Kuangaliana kwa macho ni muhimu kama njia moja wapo ya mawasiliano ya kimwili na hutumika kila wakati. Inategemea na muda ambao mwanamume atakuangalia kwa macho hivyo basi kufahamu kama anakutongoza au la. Kama atachukua muda wake mwingi hapo tayari anajaribu kugonga ndipo hivyo kama mwanamke nafasi yako ya kuchukua majukumu yanaanzia hapo. Pia kama mwanamume atachukua muda mfupi zaidi anaweza kuwa pia anajaribu kukutongoza (kwa wanaume wenye haya).

4. Kuiga
Wakati mwingine wanaume huiga matendo ya wanawake bila wao kujifahamu. Kuiga ni njia nyingine ya kutongoza ya wanaume kwa wanawake. Hii ni kuanzia kuiga mtindo wa kufumba macho, hadi mitindo ya kuongea. Kwa mfano, ukicheka na yeye pia hucheka. Enyewe ni natural kuwa mtu yeyote huiga matendo ya mwingine ambaye anampenda. Halafu fahamu kuwa kuna mitandao kadhaa ya kutongozana ambayo inaipa kipao mbele mtindo huu wa kutongoza kwa kuiga.

5. Kuweka mkono kwa kiuno
Kama utamwona akisimama na wewe huwa huweka mkono kwa kiuno ama kuweka vidole vyake mbele kwa mshipi wake, fahamu kuwa amekutamani. Hii ni njia kukuonyesha kuwa anajiamini kama mwanamume. Lakini kuna baadhi ya wanawake hawapendi aina hii ya kutongoza.

6. Kukugusa kwa njia ya kutongoza
Kama mwanamume anayekupenda atakugusa, hii ni dalili kuu kuwa anakupenda. Lakini, kama ni mguso wa bahati mbaya, jipe tym uchunguze zaidi. Inamaana kuwa mwanamume huyo anajaribu kuleta atenshen flani na anatafuta njia zaidi za kuongea na wewe. Umempenda huyo mwanamume? Kama jibu ni ndio, wangojea nini? Mrudishie na wewe. Wanawake wengi kwa uhakika hupuuza jambo hili muhimu sana, uzilipuuze hata mara moja.

7. Kukunja shingo
Jinsi mwanamume hukunja shingo yake unaweza kufahamu kama anakupenda au la. Huu mtindo wa wanaume kupelekwa vichwa karibu na wewe kutaka kukuskiliza zaidi ni njia rahisi kifahamu kama anakupenda. Lakini usiichanganye kwani yaweza pia kutumika na wanaume ambao wana matatizo ya maskio.

8. Kupanuka kwa mboni
Wakati mwingine macho yetu hutuabisha kwa mambo tusiyotaka kuonyesha. Tukiwa na watu tunaowapenda mboni zetu hufunguka na kuwa kubwa kwa kupanuka, na tukiwa na watu tusiowapenda hujeuka na kuwa ndogo. Ukiona kama mwanamume akiwa na wewe macho yake hupanuka, fahamu kuwa asilimia kubwa ni kuwa anakupenda.

9. Kope zake kuziweka juu
Mwanamume anaweza kuyaficha macho yake mkiwa mnaongea ili akufiche kuwa anakupenda.
Anaweza pia kuzipandisha kope zake ziwe juu kiasi. Kama macho yake ameyapanua halafu kope amezipandisha juu kiasi, fahamu kuwa anakutongoza. Kama bado hujaufanya huu uchunguzi basi muda wako ndio huu. Mara moja tu utagundua.

10. Kuwa na wasiwasi
Je huwa wewe huingiwa na wasiwasi kama unaongea na mwanamume unayempenda? Naamini jambo hili lishawahi kukutokea hata kama mara moja. Hii ni kawaida na sana wanawake ni wazuri kwa kitendo hiki cha kuingiwa na wasiwasi. Hii hutokea wakati unatarajia unayempenda akupe sapraiz kama anakupenda au la.
Haya yote pia humtokea mwanamume. Ukimwona ameanza kupapatika na kutoa kijasho kipajini wakati anapoongea na wewe usidhanie anakuogopa wala usione ameishiwa na mistari....huo tayari ni mstari wake wa nguvu.


Hizi ndizo baadhi ya dalili kuu kuonyesha kuwa mwanamume anakutongoza.
Je, yashawahi kukutokea mambo kama haya halafu ukayapuuza? Well, next time usimpe nafasi. Akionyesha dalili kama hizi wee mrukie...huwezi kujua kama huyo ndiye umechaguliwa.

Machapisho zaidi aina hii yanapatikana katika bkuHABARI kwa ukurasa wa MAISHA

Imeandikwa na mhariri wa bkuHABARI
Dalili 10 Za Kuonyesha Kuwa Yule Mwanamume Anakutongoza (Wanawake) Dalili 10 Za Kuonyesha Kuwa Yule Mwanamume Anakutongoza (Wanawake) Reviewed by Admin on Saturday, June 07, 2014 Rating: 5

No comments:

Tunapenda kuyasoma maoni/reaction kutoka kwako!

Kama una maoni tofauti na chapisho la hapo juu, wasiliana nasi kupitia ukurasa wetu wa mawasiliano

Powered by Blogger.