Unordered List

Definition List

Michael Jackson Kutoa Albamu Mpya, Bado Anawika Akiwa Mwendazake!

Gwiji wa nyimbo za aina ya pop Michael Jackon anapaniwa kutoa albamu yake mwezi Mei.

Staa huyu hatokuwepo kwa uzinduzi huu wa albamu mpya kwani aliaga dunia takribani miaka mitano iliyopita. Kulingana na Sony na Epic Records siku ya jana, wameweka wazi kuwa watazidua albamu ya mwendazake kwa jina Xscape.

MJ
Cover albam ya Xscape

So itakuwaje staa huyu awe na uwezo wa kutoa albamu ilhali ameaga dunia?

Hilo si tatizo kwani staa huyu ni miongoni mwa mastaa waliofariki ambao wanalipwa sana ulimwenguni kwa hivyo jambo la kutoa albamu sioni utata.

Tukiachana na hayo, kulingana na Epic CEO L.A Reid, albamu hio imekusanya nyimbo kutoka albamu za awali za staa huyu ambazo bado hazijatolewa, halafu zikafanyiwa ukarabati wa kisasa kabla kuongezewa mambo kadhaa na producer Timberland na Rodney Jerkins.

Albamu inakisiwa kutolewa Mei tarehe 13.
Michael Jackson Kutoa Albamu Mpya, Bado Anawika Akiwa Mwendazake! Michael Jackson Kutoa Albamu Mpya, Bado Anawika Akiwa Mwendazake! Reviewed by Admin on Tuesday, April 01, 2014 Rating: 5

No comments:

Tunapenda kuyasoma maoni/reaction kutoka kwako!

Kama una maoni tofauti na chapisho la hapo juu, wasiliana nasi kupitia ukurasa wetu wa mawasiliano

Powered by Blogger.