Unordered List

Definition List

Jombi Anyafuliwa Sehemu Zake Za Siri Na Fisi Ili Awe Tajiri

Mr Zulu, from Malawi, said he was told by a witch doctor that if he sacrificed some of his body parts he would become rich
Jamaa ameachwa bila nyeti na kupoteza vidole vyake vya miguu baada ya mganga wa kienyeji kumwambia kuwa akitoa baadhi ya sehemu zake mwilini angekuwa tajiri. Jombi kwa jina Chamangeni Zulu kutoka Malawi, amelazwa katika hospitali ya Chipata General Hospital nchini Zambia karibu na mpaka wa Malawi, baada ya kuachilia nyeti zake ziliwe na fisi.

Zulu aliliambia gazeti la Times of Zambia siku chache zilizopita kuwa aliahidiwa na mganga huyo kuwa kwa kutoa kafara ya baadhi ya sehemu zake za mwili angeweza kuwa tajiri wa kupindukia.

"Nilikutana na jamaa fulani ambaye amefanikiwa kibiashara na baada ya kumhoji alinipa siri ya kuwa kutaka kuwa tajiri lazima utoe sehemu zako za siri." Zulu aliliambia gazeti. "Nilipewa maagizo kuwa nilale uchi katika kichaka na fisi alikuja kuninyafua vidole vyangu vya miguu kabla kuutoa uume wangu."

Ijapokuwa jamaa huyu alifuata maagizo ya mganga huyo, hajaelewa vyema mganga huyo alipomaanisha kuwa nyeti zake zitapotea.

Kulingana na wauguzi katika hospitali hio, Zulu anaendelea kupata matibabu na yuko katika hali njema.

Baada ya kuulizwa kama bado ana matumaini ya kuwa tajiri alisema kuwa matumaini yake ni makuu kuwa atafanikiwa kimaisha ila tu wakati wake utimie.


Jombi Anyafuliwa Sehemu Zake Za Siri Na Fisi Ili Awe Tajiri Jombi Anyafuliwa Sehemu Zake Za Siri Na Fisi Ili Awe Tajiri Reviewed by Admin on Tuesday, April 01, 2014 Rating: 5

No comments:

Tunapenda kuyasoma maoni/reaction kutoka kwako!

Kama una maoni tofauti na chapisho la hapo juu, wasiliana nasi kupitia ukurasa wetu wa mawasiliano

Powered by Blogger.