Unordered List

Definition List

Adebayor: Mamangu Nimchawi Ameniroga

STRAIKA wa Klabu ya Tottenham ya nchini Uingereza, Emmanuel Adebayor amekosana na mamaake kwa madai kwamba anatumia uchawi kumharibia kazi yake.


Taarifa zinaeleza kuwa, mama huyo tayari ameondoka katika nyumba ya familia huku dadaake Adebayor aitwaye Maggie akiiambia radio moja ya mjini Accra kwamba Adebayor ndiye aliyemfukuza. Lakini mchezaji huyo wa zamani wa Arsenal anadai kwamba mama yake aliondoka mwenyewe na kwamba hawana mawasiliano yoyote kati yao kwa kuwa amekuwa akitumia uchawi kutaka kumuharibia kazi yake.

''Ninawezaje kuzungumza na mama ambaye yeye na dadaangu wamekuwa wakijaribu kuniroga'' aliwauliza maripota. Kiwango cha Adebayor katika Klabu ya Tottenham kimeathirika katika kipindi cha miezi kadhaa iliyopita huku Tottenham ikidaiwa kujaribu kumuuza kwa mkopo mchezaji huyo katika dirisha la uhamisho wa mwezi Januari kufuatia kushuka kwa kiwango chake.
Adebayor: Mamangu Nimchawi Ameniroga Adebayor: Mamangu Nimchawi Ameniroga Reviewed by Admin on Saturday, November 22, 2014 Rating: 5

No comments:

Tunapenda kuyasoma maoni/reaction kutoka kwako!

Kama una maoni tofauti na chapisho la hapo juu, wasiliana nasi kupitia ukurasa wetu wa mawasiliano

Powered by Blogger.